Climate Strike Karatu:

Tai Na Maisha Yetu

Hapo zamani mtu mmoja aliokota kinda la tai wakati akitembea porini. Alichukua kinda hilo mpaka nyumbani na kuliweka katika banda la kufugia vifaranga vya kuku. Kinda hilo la Tai lilijifunza kula na kuishi kama kuku.

Tai

Siku moja mtaalamu wa ndege alipita mahali pale na kumuuliza mwenye tai huyo ,kwanini alimchanganya mfalme wa ndege yaani  tai pamoja na vifaranga vya kuku? Mwenye tai alimjibu kwamba kwakuwa tai huyo alilishwa chakula cha kuku na alimzoesha kuishi kama kuku hivyo alikua hawezi kuruka maana hakujifunza kuruka. Aliishi kama kuku hivyo hana tabia za tai,  Lakini mtaalamu alisisitiza kwa kuwa tai huyo hana moyo wa kuku akifundishwa kuruka anaweza kuruka.

Baada ya mazungumzo ya mda watu hawa wawili walikubaliana kutafuta njia zinazoweza kutumika kumfundisha tai huyo kuruka.

 Mtaalamu huyo alimchukua tai huyo taratibu mikononi mwake kisha akasema “wewe ni wa angani si wa ardhini nyoosha mabawa yako na uruke juu.
Hata hivyo tai alifadhaika na hakuweza kujielewa  yeye alikuwa nani? na alipoona vifaranga wakila chakula chao, alitua chini na kuchanganyikana nao.

Bila kukata tamaa mtaalam alimchukua tai tena siku iliyofuata juu ya paa la nyumba na akamshurutisha tena kuruka kwa kusema “wewe ni tai ,nyoosha mabawa yako na ruka angani” Lakini Tai aliogopa kwa kutojua nafsi yake na kutua chini tena kwenye chakula cha vifaranga.

Siku ta tatu mtaalamu aliwasili asubuhi na mapema na kumchukua tai nje ya banda la vifaranga juu ya mlima mrefu . Alimshika tai na kumuweka juu kisha akamshawishi tena kwa kusema “wewe ni tai, ni lazima uwe pale unapohusika ,Wewe ni wa angani nyoosha mabawa yako na sasa ruka juu.”


Tai aliangalia pande zote akaona eneo la juu angani na tai akaanza kutetemeka , Polepole akanyoosha mabawa yake na hatimaye akatoa kilio cha kushangalia na akaruka juu na kupotelea angani.

Inawezekana kabisa kwamba tai anawakumbuka vifaranga kwa majonzi makubwa, inawezekana pia huwatembelea vifaranga katika banda lao mara kwa mara lakini tai hajaweza kurudi tena na kuishi maisha kama vifaranga.

JIULIZE

  • Namna gani hadithi ya tai inafanana na safari yako ya kujitambua/maisha?
  • Katika nafsi yako binafsi jambo gani linafanana na tai?
  • Unajisikia amani na tabia ulizonazo? ni za kwako?
  • Yupi anaweza kuwa mtaalamu wa kukusaidia katika kujitambua?

Kama tai alivopata ugumu wa kujitambua na kurudi kwenye uhalisia wake inatukuta nasisi kwenye maisha yetu kuna wakati tunajikuta tunaishi maisha ambayo si ya kwetu kutokana na kuiga uhalisia au tabia za watu waliotunguzuka.

 Wapo wanaofurahi kukuona umeanguka, huna muelekeo , hufanikiwi, wala kusogea hatua moja mbele, Mara nyingine unaweza usiamini ukiwafahamu watu hao, Lakini ni muhimu watu hawa kuwepo ili tuweze kujifunza mambo ambayo si rahisi kujifunza kwa maneno tu.

Kuna wakati tunahitaji kabisa kufanya maamuzi ya jambo fulani/maamuzi ya kubadilisha mienendo yetu lakini tunapambana na vitisho au hofu ya kuona kwamba hatutaweza …lakini mabadiliko yanaanza ndani yako ukiwa na nia ya kubadilika/ya kufanya jambo hutaogopa maumivu au vitisho vitakavyokuja baada ya kufanya maamuzi., ilimaradi majibu yamabadiliko yako yawe ni uhalisia na usahihi ndani ya maisha yako.

Wapo wanaotamani kuona wenzao wameamka tena , wamefanikiwa, wamejikwamua, wamesogea hatua moja mbele.

Kuna muda tunakutana na watu wanaoonyesha kutusaidia wakatushika, nasi yatupasa kufanya bidii kujifunza kuruka wenyewe kwasababu hatujui aliyeguswa kukusaidia, hataacha lini kukusaidia kila siku mtu huamka na wazo jipya.

::  Ni kitu gani kwenye maisha yako unahitaji kukibadilisha na kukaa kwenye uhalisia wako,.. rudia hadithi kwa makini kisha fanya maamuzi.

Sikia, Tafakari , Tofauti ni wewe

BEHAVIOUR CHANGE IS POSSIBLE

BY VALERIE NYANJE

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *