Climate Strike Karatu:

Kesho Haiwezi Kurudi Jana na Jana Haiwezi Kuwa Leo

Natumai  msemo wa wenzetu wa magharibi usemao “Time is Money” si mgeni masikioni kwetu. Yawezekana kwamba msemo huo kwa tafsiri ya moja kwa moja, unamaanisha kwamba muda ni pesa. Lakini msemo huo unajaribu tu kuonyesha jinsi gani muda ni kitu cha thamani!   

Jinsi unavyoutumia muda wako hivi leo ni ishara tosha ya matokeo ya jinsi kesho yako itakavyokuwa, kujilimbikizia vitu vingi na kutovitimiza kwa wakati kunazorotesha nguvu au mbio za mafanikio yetu, ivyo ni vema kupanga na kuifata ratiba ya muda wako vizuri kulingana na matokeo unayoyataka,.

NAMNA YA KUPANGILIA MUDA WAKO:

1. Vipaumbele

 Ni kweli kwamba una vitu vingi sana vya kufanya lakini si kweli vyote vina ulazima na umuhimu sawa ivyo katika kupanga muda wa kufanikisha vitu vyako zingatia vitu ambavyo ni kipaumbele kwanza na uvipe mda kwanza.

2. Muhimu

Kuna vitu vya muhimu katika mipango yako ya kila siku na ivyo ni vema kuviorodhesha ili vikusaidie kutopeteza muda mwingi kwa vitu visivyokua na msingi, na badala yake kutumia muda huo kuchochea mipango ya mafanikio yako.

3. Kawaida

 Kuna vitu vya kawaida kabisa kwenye maisha yetu ambavyo hata kama tusipoviweka kwenye ratiba yetu ya leo vinawezekana kufanya nkesho na visilete madhara, mfano umepenga kulala kila siku mchana kulingana na ratiba ya siku kubana na vitu muhimu basi unaweza ukabadili ratiba hiyo kwa ajili ya umuhimu wa jambo linalofanya ubadili ratiba hiyo.

4. Ziada

Hapa yatupasa kuwa makini mno, kwasababu ni mara nyingi tunadondoka kwenye safari zetu za maisha kwa kuyapa mda mwingi,.. mambo ya ziada/au yasiyo na umuhimu katika malengo yetu,. mfano unaweza ukawa unapenda mpira kiasi kwamba ukawa uko tayari hata kuacha vikao vya msingi kwaajili tu ya muda wa kuangalia mpira,. –unapenda kwenda night club sana kiasi kwamba kesho yake inakufanya uchelewe kuamka na kuchelewa kuwasili mapema kwenye sehemu ya muhimu labda kazini au kwenye ratiba zingine,.. Siwezi sema ivo vitu si vizuri ila kama kwa wakati huo kuna cha umuhimu zaidi basi kifanyike kwasababu hayo mengine yapo tu hayaishi ila muda haurudi nyuma. 

Saa_yenye_radi_ya_kung'aa

JIPANGILIE

Ukipenda unaweza kusema hili la kujipanga na kupangilia ratiba ni mkusanyiko wa yote niliyotaja hapo juu. Muda mwingi sana huwa tunaupoteza kutokana na kutopangilia vizuri mambo yetu,ratiba zetu za kila siku.

Upo umuhimu  wa kupangilia shughuli zetu kutokana na sehemu za kijiografia,ili kama unafika sehemu kukamilisha jambo moja na kumbe matatu nayo yalihitaji eneo hilohilo ikusaidie kukamilisha kwa wakati na kukuepushia kupoteza mda wa kurudi eneo hilo mara kwa mara., mfano wa kawaida umekaa jikoni unapika, umenyanyuka kwenda kuchukua mafuta umeanza kuweka jikoni unagundua kitunguu huna unanyanyuka kwenda kununua, umeanza kupika unakumbuka chumvi iliisha unanyanyuka tena,..nijambo ambalo pengine ulitaka kutumia nusu saa unatumia lisaa, Kwanini? Jibu rahisi ni ukosefu wa mpangilio.   

Mbinu za kuokoa muda ni nyingi zaidi ya hizi chache ambazo nimeziorodhesha. Unaweza kuongezea katika orodha hii ila jambo muhimu kukumbuka ni kwamba muda ni kitu cha thamani sana katika maisha yetu natunapojaribu kuutumia vibaya tunazorotesha mipango mingi katika maendeleo yetu. 

KESHO HAIWEZI KURUDI JANA NA WALA JANA HAIWEZI KUWA LEO

Valerie Nyange

SIKIA TAFAKARI TOFAUTI NI WEWE

Valerie NyangeLeave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *