Climate Strike Karatu:

Jicho La Fikra

JICHO LA FIKRA  ni jicho linaloona kwa upana wa zaidi ya uwezo wako , mfano ukifikiria kikombe aufikiriii tu kwamba kinatumika kwa kuwekea chai  bali utawaza nini kilichotumika kutengenezea, na kwanini kinawekea chai tu na si mboga?  JICHO LA FIKRA ni kufikiri kwa upana zaidi kwa kutarajia maono uliyonayo..,.

Safari sahihi ya fikra inapaswa kuanzia nje ya ubongo yani kufikiri nje ya ubongo wako,Kuna wakati ubongo wako unakupa mwisho wa uwezo wako wakutenda jambo, lakini nje ya ubongo wako unajiona sehemu kubwa na ya juu ambayo ubongo wako unakuonyesha kuwa kwa uwezo ulionao huwezi kufika unapopaona.

Ubongo Wa binadamu

Ujinga ni zao la ubongo wako mwenyewe pale unapotoa majibu yasiyo sahihi juu ya kitendawili cha maisha yako, wakati mtegaji ni wewe mwenyewe.

Akili iliyoshindwa kujitambua ni mzigo kwa maendeleo ya familia, na jamii, Na hakuna mabadiliko yanayoweza kuletwa kusipokua na mapinduzi ya fikra, hata ubunifu wa biashara, kuchagua mwenzi wa ndoa, kuishi kwenye mahusiano, Imani , pasipokua na fikra yakinifu lazima utafanya maamuzi yasiyofaa.

Kila binadamu anawazo/ono la maendeleo yake lakini kuelekeza wazo lako na watu wakakuelewa kwa kiwango kilekile unachokiona kwenye fikra zako ni ngumu, 

Hivyo unatakiwa kusimama mwenyewe kwenye fikra za maono yako na kujitetea ili kufikia lengo .


nini unahitaji kukiona katika maisha yako?
nani atakuwezesha kukiona?
Lini unahitaji kukiona?
je kazi/ biashara / elimu uliyonayo ni majibu tosha ya maono yako?
Umeanza safari ya kufikia maono yako?

Sikia, Tafakari, Tofauti ni wewe

 BEHEVIOUR CHANGE IS POSSIBLE

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *